Ijumaa, 30 Septemba 2016

JINSI YA KUTUNZA NYWELE NATURAL

Nywele natural ( ambazo hazijawekwa relaxer) zikawa au ndefu, kama zinatunzwa vizuri huwa zinafutia. Na kama ukisuka, nyoa au kuzitengeneza kwa style itakayoendana na kichwa chako, utapendwa sana.
Kutunza nywele natural na zilizowekwa dawa ni vitu viwili tofauti hivyo zingatia yafuatayo ukitaka nywele zako natural  (ndefu/fupi) ziwe katika ubora unaotakiwa;
image
MAFUTA
Tumia mafuta ya maji; kama ( ya nazi, olive oil, jojoba oil au castor oil) kwa nywele natural ni mazuri zaidi hulainisha ngozi ya kichwa, hufanya nywele zikue vizuri na kuzuia mba. Mafuta ya mgando kwa nywele natural ni rahisi sana kupata mba tofauti na nywele zenye relaxer.
KUOSHA
Unapoosha nywele ni vizuri kutumia shampoo ambayo imetengenezwa kwa ajili ya natural hair au ukitumia shampoo iliyotengenezwa kwa ajili ya nywele za relaxer jaribu kutumia shampoo yenye conditioner. Itasaidia nywele zako kuwa laini na kuzuia zisiwe kavu baada ya kuosha.
image
STEAMING
Fanya steaming ya nywele zako kwa mwezi hata mara 2, tumia steaming products kwa ajili ya natural hair au fanya steaming ya yai ni nzuri sana kwa kurutubisha natural hair. Osha nywele zako na shampoo kisha koroga yai na paka kichwani kwenye ngozi, Vaa kofia ya plastic kwa dakika 45, kisha osha vizuri.
image
KUCHANA
Nywele za kiafrika ambazo hazijawekwa dawa zina asili ya kujisokota au nyingine ni kipilipili hivyo mara nyingi zi napenda kufungana, hivyo wakati wa kuchana unabidi uwe mwangalifu zisikatike, tumia chanuo ambalo ni pana. Paka hair lotion( hair moisturizer / pink lotion) kwenye nywele na mafuta ndio uanze kuchana taratibu. Ukienda kulala jaribu kusuka mabutu na kuvaa kofia ili nywele zisijifunge au kujisokota.
image image
VITU VYA KUTUMIA
Angalia kwenye picha chini products nzuri za kutumia kwa natural hair

imageimageimageimageimage
image

0 maoni:

Chapisha Maoni