MUONEKANO mzuri unabebwa na vitu vingi sana, ikiwemo na umbile pia.
Unaweza ukajitengeneza vizuri sana lakini kitu kimoja tu kikaondoa muonekano wako mzuri.
Nyama zilizokaa kihasara hasara mwilini ni sababu nyingine tosha ya kuondoa urembo wako, kwa kuwa si mavazi mengi yanatakayokukaa mwilini.
Ni vyema kama wajipenda na kujithamini, ukajitahidi kujiweka sawa mwilini ili unaposimama kwenye kioo, uweze kujikwatua bila matatizo kuanzia ndani hadi nje ya umbile.
Hii hapa ni namna nzuri ya kuondoa nyamanyama mwilini na hususan katika maeneo ya tumbo.

Kwanza kabisa asubuhi kunywa chai nzito itakayokushibisha vyema na mchana kula chakula kilichokamilika nikimaanisha chenye virutubisho vyote.
Muda wa usiku kula matunda tu ili uweze kuupa mwili nafasi ya kujitengeneza na hasa kupunguza mafuta yaliyozidi mwilini.
Hakikisha unakula pale tu unaposikia njaam kwa kuwa wataalam wanabainisha kuwa kula bila ya kusikia njaa unasababisha mrundikano wa chakula mwilini na baadaye chakula hicho hubadilika na kuwa mafuta ambayo
hutengeneza manyama uzembe.
Kama utashindwa kupunguza nyamanyama kwa njia hiyo ya chakula, basi jitahidi zaidi katika mazoezi.Imetoka kwa mudau.
0 maoni:
Chapisha Maoni