Jumatano, 12 Oktoba 2016

Hii ni aina nne ya vyakula ambavyo ukila vinasaidia kupunguza uzito…

Moja kati ya matatizo yanayowakumba watu wengi kwa kizazi cha sasa ni tatizo la uzito , tatizo hili limekuwa chanzo cha matatizo mengine makubwa na yenye madhara makubwa kwa afya ambayo wakati mwingine husababisha kifo.
Magonjwa ya moyo, kisukari, shinikio la damu la kupanda na kushuka, matatizo ya figo na viungo vingine vya mwili pamoja na kukosa mvuto wa kawaida yanasabishwa na mtu kuwa na uzito ambao anashindwa kuumudu.
Uzito huongezeka kutokana na mtindo fulani wa maisha ya mwanadamu na pia unaweza kupungua kutokana na mtindo huu huu wa maisha ambao kama ukimudu kuuzingatia hasa kwenye chakula unaweza kupungua uzito na kuishi maisha salama.
Ifuatayo ni orodha ya vyakula vya aina nne tofauti ambavyo unaweza kuanza kuvipanga kwenye chakula chako ambavyo visaidia sana kupungua uzito.
1. Mayai
Katika miaka ya hivi karibuni tafiti nyingi ambazo si sahihi na si za kweli zimesababisha watu kutozingatia ulaji wa mayai hasa yakiwa mazima na muhimu kuliko yote ni ile sehemu ya kiini cha yai, watu wengi wameaminishwa kuwa kiini cha yai kina mafuta ambayo ulaji wake huweza kufanya mtu anenepe bila mpangilio.
Mafuta yanayopatikana kwenye kiini cha yai si mafuta mabaya bali ni yale amabyo mwili inayahitaji na hayana hatari kwa mwili wa binadamu.
Whole-eggs-sl
Kiini cha yai kina virutubisho muhimu sana kwa mwili wa mwanadamu ikiwemo protini pamoja na chembechembe zinazosaidia kupunguza sumu mwilini.
2. Chokoleti Nyeusi
Tafiti nyingine zisizo sahihi zimewaaminisha wengi kuwa chokoleti sio kitu kizuri, lakini ni kinyume chake kwani si kila chokoleti zina madhara kwa mwanadamu na baadhi yake ikiwemo zile nyeusi zina faida kubwa mwilini.
The-Benefits-of-Dark-Chocolate-for-Valentine’s-Day-Recipe-Included
70% ya chembechembe zinazotengeneza chokoleti nyeusi ni kokoa, chokoleti hii ina virutubisho pamoja na madini muhimu mwilini kama vile Magnesium pamoja namanganese ambayo husaidia mwili katika masuala mbalimbali ikwiemo kuponya vidonda na kuridishia chembechembe hai za mwili zinazopotea.
Chokoleti nyeusi pia husaidia kupunguza uwezekano wa mtu kupata maradhi ya moyo na maradhi mengine yatokanyo na shinikizo la damu.
051613-251842-cook-the-book-sardines-in-spicy-tomato-sauce
3. Samaki Wadogo ‘Dagaa’.
Samaki wadogo ambao hufahamika kama dagaa wana faida nyingi sana mwilini, sababu kubwa ya faida yao ni jinsi ambavyo wanaliwa wazima kwa maana ya ngozi yao, mifupa na vitu vyote vilivyomo ndani yake ambavyo kimsingi vina faida kubwa sana.
Dagaa wana kila kitu ambacho mwili wa mwanadamu unahitaji kwa maana ya virutubisho ambavyo vinaboresha afya na kumpa mtu nguvu pamoja na kinga dhidi ya magonjwa na pia kusaidia kuponya magonjwa pale mtu anapokuwa mgonjwa.
4. Nyama ya Ini 
Katika hali ya kawaida ile kauli ya kusema kuwa nyama nyekundu si nzuri kwa mwanadamu ina usahihi wake na ina mahali ambako si sahihi.
Usahihi wake ni kwamba, nyama nyekundu si nzuri kwa mwili wa mwanadamu, si nyama zote nyekundu si nzuri kwa mwanadamu kuna nyama ambazo ni sahihi na nyingine si sahihi.
Nyama ya ng’ombe na mbuzi zina madhara makubwa zinapoliwa kwa wingi na pasipo mpangilio.
2006-11-01-urban-bachelor-cooking-pork-liver
Lakini kuna nyama nyekundu ambazo zinahitajika mwilini na mojawapo kati ya nyama hizi ni nyama ya ini mnyama Simba ni kama anajua kuhusu hili kwa sababu Simba anapoua mnyama huanza kula viungo vyake vya ndani kabla ya kula sehemu nyingine.
Nyama ya ini virutubisho muhimu kama vile Vitamin A, madini mbalimbali kama Shaba,Zinc, Selenium, Folate na Niacin pamoja na Protini kwa kiwango kikubwa.
Virutubisho vyote hivi vina faida kubwa sana mwilini mwa mwanadamu, kula nyama ya ini hata mara moja kwa wiki ina faida kubwa sana.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza 

Maoni 1 :

  1. Online Casino Malaysia: BONUS TIPS & FS | KADG PINTAR
    Online Casino Malaysia 메리트 카지노 BONUS 메리트 카지노 주소 TIPS kadangpintar & FS | KADG PINTAR.

    JibuFuta