Uso unahitaji kutunzwa vizuri maana ndio reception ya mwili wako, matunzo ya uso hayaitaji vipodozi vya gharama ni ufuatiliaji wa vitu vidogo vidogo tu.
Osha uso wako na sabuni walau mara mbili kwa siku kuweweka katika hali ya usafi na kuondoa mafuta, vumbi, jasho nk
Usilale bila kuondoa makeup usoni maana ukifanya hivyo uwezekano wa kupata chunusi ni mkubwa sana na ngozi inachakaa haraka. Osha uso wako vizuri kuondoa makeup kabla ya kulala na kuiacha ngozi ipumue.
Unaponunua lotion, cream au sabuni hakikisha unanunua inayoendana na ngozi yako kama ni ngozi kavu au ya mafuta. Soma maelekezo kabla ya kununua, mfano sabuni au lotion zenye ndimu au limao mara nyingi ni za ngozi ya mafuta, zenye aloe vera au tango kwa ngozi zote.
Sugua uso wako na sabuni na kitaulo laini taratibu kisha unaosha walau mara moja kwa wiki kuondoa ngozi iliyokufa (dead skin) na kuiacha ngozi yako inangaa na laini. Kama ngozi yako ina mafuta mengi fanya hivyo mara mbili kwa wiki.
Ili kuwa na ngozi nyororo na inayovutia hakikisha pia una kunywa maji ya kutosha, pata usingizi wa kutosha, kula vizuri, epuka pombe kupita kiasi na sigara zitakuzeesha. Kila mtu anaweza kuwa na ngozi inayovutia.
Hapa nazungumzi matunzo ya uso ya kawaida sio kuondoa madoa na chunusi. Ukipenda kujua jinsi ya kuondoa chunusi kwa vitu asilia bonyeza Link usome, http://eunicemahundi.com/2015/02/03/jinsi-ya-kuondoa-chunusi-kwa-kutumia-vitu-asilia/
0 maoni:
Chapisha Maoni