Home
/
Unlabelled
/
USHAURI WA BURE KWA MWANAMKE TEGEMEZI
Katika harakati za kupambana na umaskini ,wanawake wengi wamekuwa wakihangaika huku na kule kutafuta kipato ambacho kinaweza kuzitunza
familia zao.
Katika harakatri hizo wapo ambao wameweza kufikia malengo yao na wapo ambao wamekata tamaaa kutokana na ugumu washughuli ambazo wao binafsi
wamezichagua na baadala ya kuwaletea mafanikio zimekuwa zikiwaletea hasara.
Hata hivyo bado wapo wanawake wengi ambao wamekuwa tegemezi kutokana na kushindwa kujishuhulishja na shuhuli ndogo ndogo ambazo
zingeweza kuwaingizia kipato kwa namna moja ama nyingine na kuweza kuyamudu mahitaji yao.
Wengi wamekuwa wakijiweka nyuma wakiamini kwamba mwanaume ndiye mwenye wajibu wa kuitunza familia, Hali hiyo imekua ikisababisha wanawake wengi kushindwa kufanya mambo mbalimbali ya maendeleo kutokana na kile wanachoachiwa kuwa kidogo ambacho hakitoshelezi.
Baadhi ya wanawake wamekua na tabia ya kukaa bila kujishuhulisha na kushindwa hata yale mahitaji ambayo wangeweza kuyatatua wakishindwa na matokeo yake kubaki kuilaumu serikali kuwa haitimizi
wajibu wake.
Wengine wamekua wakikaa kibarazani na kupiga soga ambazo zimekuwa zikiwagombanisha hasa kwa wale ambao wanakuwa wanang’ata na kupuliza ,hawa ni wale watu ambao anachukua maneno huku na kuyapeleka kule na mwishowe kusababisha ugombanishi, Ushauri wa bure kwa wanawake wa namna hii ni vyema wakajihusisha na masuala ya ujasiriamali kwa ujasiriamali umewasaidia wengi na kuwanufaisha.
0 maoni:
Chapisha Maoni