Ijumaa, 14 Oktoba 2016


 
Ngozi Kavu inahitaji uangalizi wa hali ya juu sana kwa sababu ngozi hii huwa inakabiliwa an mishari na wrinkles/mikunjo.Na hisi hutokea hasa kipindi cha baridi ambapo ngozi huwa inakua kavu na pia huwa too rough. Lakini kuna vitu unavyoweza kufanya ili kuweza kuitunza ngozi kwa kupunguza ukavu na wakati huo huo ulinzi dhidi ya kuzeeka mapema kwa ngozi.
1. Osha uso wako kila siku na sabuni ta kusafishia uso ambayo haina chemicals na kamwe usitumie sabuni ambayo itaondoa uhasilia wa mafuta kwenye ngozi yako.
2. Kila siku tumia vilainishaji ngozi wakati wa mchana na unapopaka kilainishi kwenye ngozi yako massage ngozi yako kwa mduara kwa kwenda juu na sio kuvuta au kusugua ngozi yako.
3. Unatakiwa kupaka cream kwenye ngozi yako kabla ya kwenda kulala maana ni vyema kutumia cream ambazo zina Alpha Hydroxy Acids au AHA`s ambazo zinajulikana ambazo zinatokana na vyanzo kama vile maziwa, matunda na sukari. Hizi Alpha Hydroxy Acids zinakausha, zinaua na zinaondoa tabaka la ngozi ya nje wakati zina zinalainisha ngozi mpya inayotoka.
Faida yake ni kwamba ngozi yako inaonekana kuwa nzuri na ngavu pia ngozi yako kung`aa na kuwa na rangi nzuri. Kwa pamoja AHA na Vitamin C husaidi kupunguza mishati na ishara nyingine ya aging hivyo unaweza kupata matokeo mazuri na kwa haraka kwa kutumia vilainishi au cream ambavyo vina Vitamin C wakati wa mchana na cream ambazo zina AHA wakati wa usiku.Kwa kawaida tumia bidhaa ambazo zinakua zenye moisturiser na cream.
4. Kama ngozi yako ni kavu na inaelekea kuwa na mistari na inaonekana nyekundu na inakua inauma au ina vipele unatakiwa kumuona daktari wa ngozi. Hali hii pia inaweza kusababishwa na hali ya hewa au kusababishwa na vitambaa kama vile pamba, vitu tunavyopaka kwa ajili ya kutunza ngozi au sabuni na kadhalika. 

Daktari anaweza kukushauri ni cream gani utumie kulainisha ngozi yako na kuondoa wekundu kwenye ngozi yako pia kuondoa bugudha kwenye ngozi yako kama vile kutumia vitambaa vya cotton na kuepuka Watu wengi wanapata matatizo kuwa na ya ngozi kavu hasa kutokana na hali ya hewa. Kama ni miezi ya baridi husababisha ngozi yako kuwa kavu hivyo matumizi ya mara kwa mara ya vilainishi vitasaidia ngozi yako kuwa ngavu na nyororo.

JINSI YA KUTUNZA NGOZI KAMA NI KAVU


Ngozi yenye mafuta kwa kawaida huwa inang'ara, nene na yenye rangi iliyotitia. Mara nyingi ngozi yenye mafuta mengi sana huwa na chunusi nyingi na vipelepele na mara nyingine huwa na chunusi zenye vichwa vyeusi. Katika aina hizi za ngozi mafuta hutokana na tezi za sebaceous na kuzalisha mafuta zaidi ya kiwango kinachotakiwa. Mafuta hayo husambaa katika ngozi na kuifanya iwe na mafuta mafuta. 
Sababu zinazosababisha ngozi kuwa na mafuta:
• Kuridhi.
• Lishe.
• Kiwango cha homoni mbalimbali mwilini.
• Ujauzito.
• Vidonge vya kuzuia mimba.
• Baadhi ya vipodozi .
• Hali ya unyevu (humidity) na hali ya hewa ya joto.

Namna ya kutunza ngozi zenye mafuta
Faida kubwa ya kuwa na ngozi yenye mafuta ni kuwa haizeeki kwa haraka ikilinganishwa na aina nyinginezo za ngozi. Miongoni mwa mambo yanayosaidia ili kuitunza ngozi yenye mafuta na kuiepusha na chunusi na hali isiyopendeza ni:-
1. Ngozi yenye mafuta inahitajia kusafishwa vyema kwa maji ya moto na sabuni ili kuzuia vinyweleo visizibwe na mafuta. 
2. Epusha vifaa vigumu visikwaruze uso wako na kupelekea ngozi kubanduka, kwani suala hilo husababisha tezi za mafuta kufanya kazi zaidi ili kujaza sehemu iliyopotea ya mafuta.
3. Epuka kutumia vipodozi ambavyo huifanya ngozi yako ipotze maji au kukauka. Kwani husababisha sehemu ya juu ya ngozi inyauke, na hivyo kusababisha mafuta kuziba vinyweleo na kupelekea kutokea vichwa vyeusi.
4. Jitahidi kuitunza vyema ngozi yako na kuisafisha vizuri. Jaribu kuosha uso mara mbili au tatu kwa siku. Usioshe mara nyingi kwani kufanya hivyo huufanya uso kutoa mafuta zaidi. 
5. Chagua kile unachosafishia kwa makini, jiepushe kutumia cream nzito nzito au vifaa vugumu wakati wa kuosha uso wako. Ni bora utumie sabuni za kawaida zisizokuwa na madawa. Unaweza kutumia lotion ya kuua bacteria au sabuni zisizo na dawa nyingi (lightly medicated), au sabuni zenye madini mbalimbali. Ni bora usioshe au kutumia lotion au michanganyiko yenye alkoholi. 
6. Tumia maji ya moto au ya vuguvugu wakati unaosha uso wako. 
7. Wakati unapoosha uso wako, ukande kwa kutumia ncha za vidole, jiepushe kupaka sabuni moja kwa moja usoni, inaweza kuganda na kuzuia vinyweleo kuziba. 
8. Kutumia mask za udongo (clay) na tope (mud) husaidia katika ngozi za aina hii. Ni bora utumie mask mara moja au mbili kwa wiki. 
9. Jitahidi kutumia vipodozi vya uso ambavyo vimetengenezwa kwa ajili ya ngozi yenye mafuta.

Ngozi zenye mafuta na jinsi ya kuzitunza

Jumatano, 12 Oktoba 2016

Katika   harakati za kupambana na umaskini ,wanawake  wengi  wamekuwa wakihangaika huku na kule kutafuta kipato ambacho kinaweza kuzitunza
familia zao.

Katika harakatri hizo wapo ambao wameweza kufikia malengo yao  na wapo ambao  wamekata tamaaa kutokana na ugumu washughuli ambazo wao binafsi
wamezichagua  na baadala ya kuwaletea mafanikio zimekuwa zikiwaletea hasara.black-group-of-female-friends-pf

Hata hivyo  bado wapo wanawake wengi  ambao wamekuwa tegemezi kutokana na kushindwa kujishuhulishja na shuhuli ndogo ndogo ambazo
zingeweza kuwaingizia  kipato kwa namna moja ama nyingine na kuweza kuyamudu mahitaji yao.

Wengi wamekuwa wakijiweka  nyuma  wakiamini kwamba  mwanaume ndiye mwenye wajibu wa kuitunza familia, Hali hiyo imekua ikisababisha wanawake  wengi kushindwa kufanya mambo mbalimbali ya maendeleo kutokana na kile wanachoachiwa  kuwa kidogo ambacho hakitoshelezi.

Baadhi ya  wanawake  wamekua na tabia ya  kukaa bila kujishuhulisha na kushindwa hata yale mahitaji ambayo wangeweza  kuyatatua wakishindwa na matokeo yake  kubaki kuilaumu serikali  kuwa  haitimizi
wajibu wake.

Wengine  wamekua  wakikaa kibarazani  na kupiga soga ambazo  zimekuwa zikiwagombanisha hasa kwa wale ambao wanakuwa wanang’ata na kupuliza ,hawa ni wale watu ambao anachukua maneno huku na  kuyapeleka  kule na mwishowe kusababisha  ugombanishi, Ushauri wa bure kwa wanawake wa namna hii ni vyema wakajihusisha na masuala ya ujasiriamali kwa ujasiriamali umewasaidia wengi na kuwanufaisha.

USHAURI WA BURE KWA MWANAMKE TEGEMEZI

MUONEKANO mzuri unabebwa na vitu vingi sana, ikiwemo na umbile pia.

Unaweza ukajitengeneza vizuri sana lakini kitu kimoja tu kikaondoa muonekano wako mzuri.

Nyama zilizokaa kihasara hasara mwilini ni sababu nyingine tosha ya kuondoa urembo wako, kwa kuwa si mavazi mengi yanatakayokukaa mwilini.

Ni vyema kama wajipenda na kujithamini, ukajitahidi kujiweka sawa mwilini ili unaposimama kwenye kioo, uweze kujikwatua bila matatizo kuanzia ndani hadi nje ya umbile.

Hii hapa ni namna nzuri ya kuondoa nyamanyama mwilini na hususan katika maeneo ya tumbo.


Kwanza kabisa asubuhi kunywa chai nzito itakayokushibisha vyema na  mchana kula chakula kilichokamilika nikimaanisha chenye virutubisho vyote.

Muda wa usiku kula matunda tu ili uweze kuupa mwili nafasi ya kujitengeneza na hasa kupunguza mafuta yaliyozidi mwilini.

Hakikisha unakula pale tu unaposikia njaam kwa kuwa wataalam wanabainisha kuwa kula bila ya kusikia njaa unasababisha mrundikano wa chakula mwilini na baadaye chakula hicho hubadilika na kuwa mafuta ambayo
hutengeneza manyama uzembe.

Kama utashindwa kupunguza nyamanyama kwa njia hiyo ya chakula, basi jitahidi zaidi katika mazoezi.Imetoka kwa mudau.

Ondoa nyama uzembe kwa muonekano bomba!

Moja kati ya matatizo yanayowakumba watu wengi kwa kizazi cha sasa ni tatizo la uzito , tatizo hili limekuwa chanzo cha matatizo mengine makubwa na yenye madhara makubwa kwa afya ambayo wakati mwingine husababisha kifo.
Magonjwa ya moyo, kisukari, shinikio la damu la kupanda na kushuka, matatizo ya figo na viungo vingine vya mwili pamoja na kukosa mvuto wa kawaida yanasabishwa na mtu kuwa na uzito ambao anashindwa kuumudu.
Uzito huongezeka kutokana na mtindo fulani wa maisha ya mwanadamu na pia unaweza kupungua kutokana na mtindo huu huu wa maisha ambao kama ukimudu kuuzingatia hasa kwenye chakula unaweza kupungua uzito na kuishi maisha salama.
Ifuatayo ni orodha ya vyakula vya aina nne tofauti ambavyo unaweza kuanza kuvipanga kwenye chakula chako ambavyo visaidia sana kupungua uzito.
1. Mayai
Katika miaka ya hivi karibuni tafiti nyingi ambazo si sahihi na si za kweli zimesababisha watu kutozingatia ulaji wa mayai hasa yakiwa mazima na muhimu kuliko yote ni ile sehemu ya kiini cha yai, watu wengi wameaminishwa kuwa kiini cha yai kina mafuta ambayo ulaji wake huweza kufanya mtu anenepe bila mpangilio.
Mafuta yanayopatikana kwenye kiini cha yai si mafuta mabaya bali ni yale amabyo mwili inayahitaji na hayana hatari kwa mwili wa binadamu.
Whole-eggs-sl
Kiini cha yai kina virutubisho muhimu sana kwa mwili wa mwanadamu ikiwemo protini pamoja na chembechembe zinazosaidia kupunguza sumu mwilini.
2. Chokoleti Nyeusi
Tafiti nyingine zisizo sahihi zimewaaminisha wengi kuwa chokoleti sio kitu kizuri, lakini ni kinyume chake kwani si kila chokoleti zina madhara kwa mwanadamu na baadhi yake ikiwemo zile nyeusi zina faida kubwa mwilini.
The-Benefits-of-Dark-Chocolate-for-Valentine’s-Day-Recipe-Included
70% ya chembechembe zinazotengeneza chokoleti nyeusi ni kokoa, chokoleti hii ina virutubisho pamoja na madini muhimu mwilini kama vile Magnesium pamoja namanganese ambayo husaidia mwili katika masuala mbalimbali ikwiemo kuponya vidonda na kuridishia chembechembe hai za mwili zinazopotea.
Chokoleti nyeusi pia husaidia kupunguza uwezekano wa mtu kupata maradhi ya moyo na maradhi mengine yatokanyo na shinikizo la damu.
051613-251842-cook-the-book-sardines-in-spicy-tomato-sauce
3. Samaki Wadogo ‘Dagaa’.
Samaki wadogo ambao hufahamika kama dagaa wana faida nyingi sana mwilini, sababu kubwa ya faida yao ni jinsi ambavyo wanaliwa wazima kwa maana ya ngozi yao, mifupa na vitu vyote vilivyomo ndani yake ambavyo kimsingi vina faida kubwa sana.
Dagaa wana kila kitu ambacho mwili wa mwanadamu unahitaji kwa maana ya virutubisho ambavyo vinaboresha afya na kumpa mtu nguvu pamoja na kinga dhidi ya magonjwa na pia kusaidia kuponya magonjwa pale mtu anapokuwa mgonjwa.
4. Nyama ya Ini 
Katika hali ya kawaida ile kauli ya kusema kuwa nyama nyekundu si nzuri kwa mwanadamu ina usahihi wake na ina mahali ambako si sahihi.
Usahihi wake ni kwamba, nyama nyekundu si nzuri kwa mwili wa mwanadamu, si nyama zote nyekundu si nzuri kwa mwanadamu kuna nyama ambazo ni sahihi na nyingine si sahihi.
Nyama ya ng’ombe na mbuzi zina madhara makubwa zinapoliwa kwa wingi na pasipo mpangilio.
2006-11-01-urban-bachelor-cooking-pork-liver
Lakini kuna nyama nyekundu ambazo zinahitajika mwilini na mojawapo kati ya nyama hizi ni nyama ya ini mnyama Simba ni kama anajua kuhusu hili kwa sababu Simba anapoua mnyama huanza kula viungo vyake vya ndani kabla ya kula sehemu nyingine.
Nyama ya ini virutubisho muhimu kama vile Vitamin A, madini mbalimbali kama Shaba,Zinc, Selenium, Folate na Niacin pamoja na Protini kwa kiwango kikubwa.
Virutubisho vyote hivi vina faida kubwa sana mwilini mwa mwanadamu, kula nyama ya ini hata mara moja kwa wiki ina faida kubwa sana.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza 

Hii ni aina nne ya vyakula ambavyo ukila vinasaidia kupunguza uzito…

1.Acha kula chakula chochote chenye jamii ya sukari kwa muda wa wiki 10. 

2. Fanya mazoezi kabla hujala kitu chochote mwilini. Dakika ishirini zinatosha. Utachoma mafuta mengi zaidi tofauti na ukifanya mazoezi baada kula.

3. Beba vyuma. Hayo ndio mazoezi yatakayokusaidia kutimiza hilo lengo ndani ya wiki kumi. Kukimbia ni mazoezi ya wanawake.

4. Vyakula vyako vitakuwa ni jamii ya protini na mafuta. Mfano-nyama nyekundu[sio mchuzi wa nyama], mayai ya kuchemshwa,maparachichi,korosho,karanga,kuku(sio wa kukaanga),samaki...............

Najua wengi wenu wa mnaofanya kazi maofisni mnapenda kula mananasi,maembe,matikiti,machungwa,chapati,maandazi,chipsi,chipsi mayai,Pepsi cola, Coca cola,juisi ya matunda iliyojaa sukari,ceres,debonairs,vitumbua n.k..

Watu mnasema mafuta yananenepesha. Kwamba eti binadamu asile nyama nyekundu, au nyama ya aina yeyote ile. Mwili wa binadamu haujatengenezwa kutunza mafuta mwilini. Sema huo mwili wako na wangu unapenda kutunza sukari. Sukari ndio inayotunza mafuta. 

Kwahiyo,kwa mfano,kama unakula kitimoto na kushushia na safari moja baridi,elewa kwamba kitambi chako kinatokana na sukari iliyomo kwenye bia. Hiyo sukari ndio itakayotunza hayo mafuta ya kitimoto kwa kiwango kikubwa katika mwili wako. Nimefuata hii protocol kwa muda zaidi ya wiki kumi. Nakuahidi ya kwamba,ukiacha kula sukari ,HAITAWEZAKANA kwa mwili wako kutunza mafuta yaliyopo kwenye ki-pipa chako. Hayo mafuta yatashuka tu. 

Kwa msaada zaidi nenda:Getalife.com. Ingia kwenye section ya nutrition na soma kila kitu humo ikiwemo hii post- fat loss diet 101. Huu ndio ushauri nilioufuata mimi na umenisaidia.

Jinsi ya kukata nyama za tumboni kwa wewe mwenye kitambi-kwa mwanaume

Ijumaa, 30 Septemba 2016

chumvi ni kiungo muhimu kwa kila mlo pia inaumuhimu mkubwa katika urembo. je una fahamu kwamba chmvi unaweza kuitumia kama scurb na kukuacha ukiwa na ngozi ya kuvutia na nyororo?
matatizo ya chunusi , ukavu katika ngozi, mafuta usoni na hata ngozi iliyokufa usoni ni miongoni mwa mambo yanayowakera warembo wengi  na hatimaye kuwafanya watumie vipodozi ambavyo si salama kwa ngozi zao.
kwa kulitambua hilo wataalamu wa urembo wa asili wamegundua kuwa chumvi ni scrub yenye gharama nafuu



                                                                    CHUMVI

Ambayo kila mtu anaweza kutumia tofauti na urembo mwingine wa ngozi. matumizi ya chumvi yamekuwa na matokeo mazuri katika matatizo mbalimbali ya ngozi japo kuwa si wengi wanalolifahamu hili unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha chumvi haiingii machoni pindi unapotumia




MAHITAJI

Chumvi ya unga kijiko kimoja cha chakula

jinsi ya kufanya

nawa uso wako kwa maji safi ya kawaida kisha chukua kitambaa laini na safi chovya kwenye chumvi kisha sugua kwenye uso taratibu pia unaweza kutumia hata mwilini.

baada ya kujipaka katika uso weka pembeni kitambaa kisha anza kujisungua kwa kutumia viganja vya mikono yako fanya hivyo hadi utakapoona taka zinatoka kisha kaa kama dakika 2/5 ukisha maliza osha kwa maji ya baridi 

Ni muhimu kufanya zoezi hili kwa wiki mara mbili kwani linasaidia kuondoa mikunjo na husafisha ngozi kabisa

TUMIA CHUMVI KUONGEZA UREMBO0 WA NGOZI YAKO